Psalms 34

Sifa Na Wema Wa Mungu

(Zaburi Ya Daudi, Alipojifanya Mwendawazimu Mbele Ya Abimeleki, Ambaye Alimfukuza, Naye Akaondoka)


1
Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
bNitamtukuza Bwana nyakati zote,
sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.

2 cNafsi yangu itajisifu katika Bwana,
walioonewa watasikia na wafurahi.

3 dMtukuzeni Bwana pamoja nami,
naam, na tulitukuze jina lake pamoja.


4 eNilimtafuta Bwana naye akanijibu,
akaniokoa kwenye hofu zangu zote.

5 fWale wamtazamao hutiwa nuru,
nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.

6 gMaskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia,
akamwokoa katika taabu zake zote.

7 hMalaika wa Bwana hufanya kituo
akiwazunguka wale wamchao,
naye huwaokoa.


8 iOnjeni mwone kwamba Bwana ni mwema,
heri mtu yule anayemkimbilia.

9 jMcheni Bwana enyi watakatifu wake,
kwa maana wale wamchao
hawapungukiwi na chochote.

10 kWana simba wenye nguvu
hutindikiwa na kuona njaa,
bali wale wamtafutao Bwana
hawatakosa kitu chochote kilicho chema.


11 lNjooni, watoto wangu, mnisikilize,
nitawafundisha kumcha Bwana.

12 mYeyote kati yenu anayependa uzima
na kutamani kuziona siku nyingi njema,

13 nbasi auzuie ulimi wake na mabaya,
na midomo yake kutokana na kusema uongo.

14 oAache uovu, atende mema,
aitafute amani na kuifuatilia.


15 pMacho ya Bwana huwaelekea wenye haki,
na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.

16 qUso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu,
ili kufuta kumbukumbu lao duniani.


17 rWenye haki hulia, naye Bwana huwasikia,
huwaokoa katika taabu zao zote.

18 s Bwana yu karibu na waliovunjika moyo,
na huwaokoa waliopondeka roho.


19 tMwenye haki ana mateso mengi,
lakini Bwana humwokoa nayo yote,

20 uhuhifadhi mifupa yake yote,
hata mmoja hautavunjika.


21 vUbaya utamuua mtu mwovu,
nao adui za mwenye haki watahukumiwa.

22 w Bwana huwakomboa watumishi wake,
yeyote anayemkimbilia yeye
hatahukumiwa kamwe.
Copyright information for SwhKC